TANGAZO LA KUITWA KWENYE MAFUNZO UHAMIAJI

TANGAZO LA KUITWA KWENYE MAFUNZO UHAMIAJI 13-04-2026

Hili hapa tangazo la kuitwa kwenye mafunzo Kamishna Jenerali wa Uhamiaji anawatangazia vijana walioomba Ajira na kuitwa kwenye usaili kupitia Mfumo wa e-Ajira wa Uhamiaji kwamba wale waliochaguliwa wametumiwa ujumbe kupitia barua pepe na simu zao kuwa wanatakiwa kujiunga kwa ajili ya Mafunzo ya Awali ya Askari wa Uhamiaji ambayo yatatolewa katika Chuo cha Uhamiaji cha Raphael Kubaga kilichopo Wilaya ya Mkinga Mkoa wa Tanga. Ujumbe huo umeanisha siku, tarehe na muda wa kuripoti chuoni.

Wakati wa kuripoti Chuoni mhusika atalazimika kuonesha ujumbe wa simu au barua pepe ya wito wa kujiunga na mafunzo husika. Aidha, vijana hao wanatakiwa kuwa na Uthibitisho wa kuwa yeye ndiye mhusika halisi kama vile Kitambulisho cha Taifa, Kitambulisho cha Mkaazi au Pasipoti ya kusafiria. Sambamba na hilo, mhusika anatakiwa kuwa na nyaraka halisi za Cheti cha kuzaliwa, vyeti vya taaluma, Kitambulisho cha taifa pamoja na nakala zake.
TANGAZO LA KUITWA KWENYE MAFUNZO UHAMIAJI

TANGAZO LA KUITWA KWENYE MAFUNZO UHAMIAJI
 
Similar content Most view View more
Back
Top Bottom