Kufuatia changamoto ya kimfumo iliyojitokeza kwa baadhi ya waombaji wa nafasi za ajira za Uhamiaji ngazi ya Shahada, Idara inapenda kuwajulisha kwamba changamoto hiyo tayari imetatuliwa. Hivyo, waombaji wanashauriwa kuendelea kutuma maombi yao kupitia mfumo. Aidha, Idara inaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.